SEKTA YA MADINI
UTANGULIZI
Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi (inayojumuisha Ofisi ya Madini-Mbeya pamoja na Ofisi ya Afisa Mkazi wa Madini-Chunya) ni moja kati ya Ofisi kumi (10) za Kanda zinazosimamia shughuli za madini nchini Tanzania. Ofisi hii inasimamia shughuli za madini katika mikoa ya Mbeya na Iringa.
Majukumu ya Ofisi ni usimamiaji wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2010 pamoja na usimamizi wa Sheria ya Baruti ya Mwaka 1963 na Kanuni zake za Mwaka 1964. Miongoni mwa shughuli hizo zinazofanywa kwa mujibu wa sharia tajwa hapo juu ni pamoja na ukaguzi wa migodi mikubwa na midogo, ukaguzi wa maghala ya baruti, utoaji wa leseni mbali mbali ambazo ni uchimbaji, biashara ya madini na zinazohusiana na masuala ya baruti pamoja na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na shughuli za madini.
Vilevile, Ofisi hutoa mafunzo mbalimbali ya uchimbaji salama, utunzaji wa mazingira pamoja na biashara ya madini kwa wachimbaji waliopo katika Kanda.
Tafiti mbalimbali zimebaini uwepo wa madini mbalimbali katika Kanda. Baadhi ya madini hayo ni Dhahabu, Niobium, Makaa ya Mawe, Chokaa, Shaba, Travetine, n.k.
Kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015, Jumla ya leseni 136 za uchimbaji mdogo, leseni 2 za biashara kubwa ya madini (Dealer’sLicence) pamoja na leseni 31 za biashara ndogo ya madini (BrockersLicence) zimetolewa.
Vilevile, vibali 16 vya kulipua baruti (BlastingCertificates) pamoja na vibali vya kusafirishia na kununua baruti 28 (Licencetopurchase/AcquireExplosives) vilitolewa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa