Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amemtaka Afisa Madini Mkazi Wilaya ya Chunya kubandika bei ya soko la madini kila inapobadilika kwenye migodi yote ya wachimbaji wadogo ili waweze kuepuka kudhulumiwa madalali wa madini.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na wachimbaji wadogo wa Isoko wilayani Chunya na kusema kuwa bei ambayo wachimbaji wadogo wanauza kwa madalali (brokers) imekuwa ni ndogo kuliko ya sokoni
“tarehe 2/05/2019 tulifungua soko la madini pale Chunya mjini, tulipofungua tulitegemea watu wakauzie madini pale lakini bado kumekuwa na tabia kuja kuwadalalia hapa wachimbaji wadogo wadogo, bei iliyopo sokoni na wewe unayeuza hapa inakuwa ni Mbingu na Ardh”. Mhe Chalamila
Amesema kuwa wanachofanya madalali hao ni unyanyasaji na unyonyaji na ni utapeli ambao hautawezwa kuendelezwa katika Mkoa wa Mbeya na kuwaomba madalaliambao wanakuja kununua madini kwa wachimbaji wadogo na kuwauzia wanunuzi kutowanyanyasa na kuwaonea wachimbaji wadogo. ,
Naye Mchimbaji Mdogo Bw. Ahobokile Mwasyeba mbali na kupongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya kufungua soko hilo alieleza manufaa ya soko hilo kuwa ni pamoja upatikanaji wa wanunuzi wa uhakika wa madini hayo na bei elekezi inayotolewa na Serikali
Ahombwile ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa soko la madini bei ya gramu moja ya dhahabu haijawahi kupungua chini ya 90,000 tofauti na awali ambapo walikuwa wanauza kwa bei ya hasara.
Naye Akizungumza Mmiliki wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Mdimi Investment C. Limited, Mdimi Msigwa leo, Serikali imeweka mazingira rafiki na salama kwa wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kwa kuwaanzishia masoko ya madini, hivyo hakuna haja ya kutorosha madini.
Msigwa alieleza kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo alikuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wachache kutokana na dhahabu yake kutokuwa na soko la uhakika na kuongeza kuwa baada ya uanzishwaji wa soko aliweza kuongeza ajira kutokana na biashara ya madini ya dhahabu kuwa ya uhakika.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa