Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ametoa msaada wa fedha taslimu kiasi cha sh. Milioni moja (1,000,000) kwa Bibi Vumilia Mwakyoma aliyemwagiwa tindikali kwa ajili ya matibabu ya majeraha aliyopata.
Akitoa msaada huo hii leo ofisini kwake Mhe Makalla amemtaka Bibi Mwakyoma kutumia fedha hizo kwa Malengo yaliyokusudiwa ya ununuzi wa dawa na kumtaka atambue kuwa amepata ulemavu na kukubaliana na hali yake.
Mhe. Makalla ameitaka Mwakyoma kumtanguliza Mungu katika kila jambo na kusema kuwa kila mtu ni mlemavu mtarajiwa hivyo tunatakiwa kuangalia nyuma kwa imani na kutazama mbele kwa matumaini.
Aidha, Mhe Makalla ametoa onyo kwa tabia ya baadhi ya asasi zisizo za kiserikali kutumia wtu walio na ulemavu kama fursa ya kujiingizia kipato katika asasi zao na kuanza kufuatilia ahadi kama ni madeni ya asasi zao.
Akipokea msaada huo bibi Mwakyoma amemshukuru sana na kusema utamsaidia kupita matibabu na kumwaomba Mkuu wa Mkoa kumsaidia kufuatilia watuhumiwa waliofanya kitendo kile wakamatwe.
Bibi Vumilia Mwakyoma alimwagiwa tindikali na mtu anayedhaniwa kuwa ni mke wa mzazi mwenzie kwa wivu wa mapenzi katika Jiji la Mbeya
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa