Mwenge wa Uhuru 2024 kupitia kwa kiongozi wake Ndg: Godfrey Mnzava umetembelea na kukagua Mradi wa upandishaji Hadhi Barabara ya Ndulilo-Itete yenye Kilomita 11.35 kwa Kiwango Cha Lami unaotekelezwa na Mkandarasi M/S HARI SINGH & SONS LTD ulioko Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Mradi huu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya(European Union) anaotekelezwa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo Bajeti yake iliyopangwa ni 8,970,486,490 na Mkandarasi tayari ameshalipwa kiasi Cha 1,790,969,066.
Mrada Ulianza Kutekelezwa Tarehe 01/09/2023 na ulipangwa Kukamilika Tarehe 31/08/2024 muda wa Miezi 12 sawa na Mwaka Mmoja.
Taarifa ya Meneja wa TARURA Mkoa imesema Lengo la kipandisha hadhi kwa Barabara hii ni kurahisisha Usafiri na usafirishaji wa mizigo na mazao kwa Wananchi na Kukamilika kwa Mradi huu utawanufaisha zaidi Wananchi wa Kata za kyimo na Lufingo na Utahudumia wananchi wapatao 31,354.
Godfrey Mnzava ametoa Nasaha kwa Wananchi Wilayani Rungwe kadharika kwa TARURA kuhakikisha Wananchi wanapatiwa huduma Stahiki kwa Manufaa Mapana ya Nchi kadharika Wananchi wameaswa kulinda na kuitunza Miradi hiyo hiyo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa