Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera amefanya kikao na wadau mbalimbali wa Tumbaku Wilayani Chunya Mkoani Mbeya na kujadili masuala mbalimbali ya Tumbaku na changamoto zinazowakabili vyama vya Ushirika wa Tumbaku ili kuweza kuwanufaisha na zao hilo Wilayani Chunya, ambapo kumekuwa na changamoto ya vyama kutolipwa fedha zao kwa wakati kulingana na makubaliano na wanunuzi.
Homera amewataka wadau wa Tumbaku kuacha kuchanganya madaraja kwa wanunuzi, ametangaza kiama kwa walanguzi wanaoumiza wakulima wa tumbaku wilayani Chunya na yeyote atakayekamatwa analangua tumbaku mali itakuwa ya Serikali. Maelekezo hayo ameyatoa kwa wakuu wa vyama vya ushirika Wilayani Chunya.
“Marufuku kuchukua tumbaku, kamati ya usalama na bodi ya Tumbaku wekeni mkakati ili kampuni iweke pesa mbele tumbaku ndio ifuate, hakuna kuchukua tumbaku mpaka pesa iwekwe benki kinyume na hapo hatua zitachukuliwa kwa kamati ya usalama pamoja na bodi ya Tumbaku” Alisema Rc Homera
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa