Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Halmashauri ya Chunya kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari .
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na Wananchi wa Kata ya Makongorosi kuwa serikali tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 4 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa mkoa mzima wa Mbeya.
“ Serikali ipo katika mikakati ya kuhakikisha watoto wanapata elimu nzuri nchini kote Tanzania kwa kuendelea kuboresha miradi ya elimu. “ Chalamila
Aidha, Mhe Chalamila amesema sambamba kuongeza kasi ya kukamilisha vyumba vya madarasa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha anaongeza idadi ya walimu kulingana na uwingi wa wanafunzi katika madarasa.
Mh.Albert Chalamila amefanya ziara katika halmashauri ya wilaya Chunya na kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Isangawana
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa