Mwenge wa Uhuru 2024 kupitia kwa Kiongozi wake Ndg: Godfrey Mnzava ukiwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya umeridhia kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Daraja(Iyela Boksi Kalvat) lenye urefu wa Mita 10 na upana wa Mita 7.4 lililopo katika Barabara ya Airport-Darajan Kata ya Iyela linalounganisha Halmashauri mbili(Jiji la Mbeya na Wilaya ya Mbeya)
Daraja Hilo limegharamiwa na Fedha za Tozo ya Mafuta (Fuel Levy) kiasi Cha TSH: 302,877,560 (Milioni Mia Tatu na mbili mia Nane sabini na Saba Elfu mia Tano sitini Tu) na tayari Mkandarasi wa Ujenzi ameshalipwa Fedha yote asilimia 100.%
Meneja wa TARUA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Boniface Kasambo kwenye Taarifa yake Amesema Uwepo wa Mradi huo utawasaidia Wananchi kurahisisha Usafiri na usafirishaji wa haraka kwa Wananchi wanaohitaji huduma za Kijamii katika Kata za Iyela na Swaya na Kata za pembezoni
Kadharika Amesema Mradi huo utarahisisha Utoaji huduma ya usafirishaji wa haraka wa Mazao kutoka Kata Moja kwenda Nyingine lakini pia itachochea Shughuli za kiuchumi, ajira na Kipato kwa Wananchi wa Kata hizo mbili na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa Ujumla.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Godfrey Mnzava Amesema furaha na Amani ya Serikali ni kuona Wananchi wanapata Mahitaji Yao ya Msingi na kutokwamishwa na Kikwa chochote hasa wawapo katika Shughuli zao za Utafutaji Kipato.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa