Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune amezitaka kaya zote zinazowezeshwa na Mpango Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kujishughulisha na ufugaji wa Kuku pamoja na Bata wa asili kwani mifugo hiyo inastahimili magonjwa, soko lake ni kubwa na ufugaji wake hauna changamoto nyingi kama ilivyo kwa mifungo mingine.
Mhe. Mfune ameyasema hayo siku ya tarehe 02/03/2021 alipofanya ziara ya kuzitembelea kaya hizo katika Kata ya Ubaruki Kijiji cha Mpakani ili kusikiliza kero zinazowakabili sambamba na kujionea hatua za maendeleo walizofikia mara baada ya kuwezeshwa na mfuko huo.
“Kikubwa kilichonileta ni kuja kuwatembelea na kuwapa salamu za Serikali. Serikali itaendelea kuwawezesha kwani kwa kiasi kikubwa wale wote ambao wamekuwa wakitumia fursa hii vizuri, wameendelea kufanya vitu vikubwa zaidi. Endeleeni kujifunza na kutafuta shughuli nyingine, kwani kufanya hivyo kutawafikisha mbali.”
“Nimefurahi kuona mafanikio yenu, kila mtu kuna hatua ambayo amepiga, kuna wengine wamekarabati nyumba zao, wengine wanafuga mifugo na wengine wanajihusisha na ujasiriamali mdogo mdogo.”
“Changamoto ya magonjwa ya mifugo tutuwasaidia sababu wataalumu wapo. Kuhusiana na changamoto ya wizi nakwenda kulifanyia kazi, na nikiwa nalifanyia kazi muendelee kujilinda. Kwa wale ambao wana maeneo ya kutosha mujaribu kujiwekea wigo za maua, miba au hata tofari kwenye nyumba zetu.” Alisema Mhe Mfune
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Mpakani Bwana Amos Mgongolwa amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kwenda kuwatembelea, kusikiliza changamoto pamoja na kujionea mafanikio waliyofikia wanufaika wa kijiji cha Mpakani ambao wanawezesha na mfuko wa TASAF.
Wanufaika wa mfuko huo wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea kwani kufanya hivyo kumewaongezea ari ya kufanya vizuri zaidi na wameahidi kufanyia kazi ushauri pamoja na maelekezo waliyopewa ili waweze kusonga mbele.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa