Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla awataka viongozi wakuteuliwa kufanyiwa tathmini kujua uhamasishaji waliofanya kuhusu ujenzi wa Vituo vya Afya kila Kata na Zahanati kila Kijiji Ilani, Viwanda pamoja na masuala ya Elimu katika Mkoa kama ya Chama cha Mapinduzi.
Akiongea katika Ufunguzi wa Kikao cha Afya Mkoa Mhe. Makalla amesema utekelezaji wa Afya ya Msingi unasuasua ambapo hadi kufikia Septemba 2017, Mkoa una Vituo vya tiba 310 vikijumuisha Hospitali 15, Vituo vya Afya 25 na Zahanati 270 ambapo Zahanati 37 zipo katika Jiji la Mbeya.
Mhe. Makalla amesema kuwa Mkoa una jumla ya vijiji 553 na idadi ya Zahanati ni 233 sawa na asilimia 43.7 ya idadi ya vijiji. Aidha, mkoa una Kata 178 na vituo vya afya vilivyopo ni 25 sawa na asilimia 14 ya idadi ya Kata
Mhe. Makalla amesema kuwa wa mujibu wa Sera ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ya mwaka 2007 inaelekeza kila kijiji kiwe na zahanati na kila Kata iwe na kituo cha afya. Afya ya Msingi ikiboreshwa inasaidia kupunguza muda mwingi ambao mwananchi anatumia kutafuta huduma za afya kwa sababu vijiji vingi havina Zahanati.
“Viongozi wa Wilaya na Halmashauri mnatakiwa Kuhamasisha uboreshaji wa afya ya Msingi kwa wananchi kwa sababu ni mojawapo ya vipaumbele vya Mkoa. Wananchi hawajahamasishwa vya kutosha kuhusu ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati na Serikali ipo tayari kuweka harambee katika kila zahanati zinazohitaji kupauliwa”
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Yahya Msuya amesema kuwa moja ya malengo ya Kikao hiki ni kuweka mkazo wa ujenzi wa Vituo vya afya kila Kata na na Zahanati kila Kijiji ili kuendana sawa na vipaumbele vya Mkoa katika kuboresha Afya ya Msingi.
Dkt. Yahya Msuya amesema kuwa Mkoa lengo la Mkoa ni kujenga zahanati 4 na vituo vya afya 2 katika kila Halmashauri kwa mwaka ili kuondoa upungufu huo. Hadi kufikia Oktoba 2017 jumla ya Zahanati 7 kati ya 103 zimekamilika (Mbeya Jiji 1, Chunya 3, Mbeya DC 1, na Mbarali 2) na zahanati 96 zipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa