Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt.Juma Z. Homera amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Maji Chimala kuukamilisha kwa Wakati uliopangwa na hatatamani kusikia kisingizio Cha aina yeyote kwakuwa muda ulishaongezwa nyuma lakini Mradi bado haujamalika.
Aidha RC Homera amemuagiza pia Meneja wa Wakala ya Maji Vijinini RUSAWA Mkoa wa Mbeya Engineer Hansi Kusimamia Miradi huo unaotarajiwa kuhudumia Watu wapatao 41,376 kuhakikisha unakamilika katika muda tajwa licha ya Kwamba mpaka Sasa ni asilimia 35 pekee ambazo mradi umefikia.
"Mimi ninachokitaka Mradi ukamilike Wananchi wapate huduma ya Maji na si vinginevyo maana hii ndio dhamila Njema ya Rais wetu Dkt, Samia kuwahudumia Wananchi wa Mbarali hasa Chimala" Amesema Dkt, Homera
Mradi wa Maji Chimala Wenye Uwezo wa kuzalisha lita 2,159,747 na kuhudimia Wananchi wa vijiji Sita vya Kata ya Chimala ambavyo ni Chimala, Lyambogo,Isitu,Igumbilo, Mengele na Muwale unatarajiwa kugharimu Kiasi Cha Shilingi 4,545,480,982 mpaka utakapokamilika.
Wananchi wa Kata ya Chimala mbali na Kuomba Serikali kuwatazama kwa jicho la Tatu kihuduma lakini pia wamempongeza Dkt, Samia kwa kitu yake ya kuwapambania wana-Mbarali hasa kuwajengea miundombinu ya kutosha ikiwemo ya Elimu, Afya,Barabara na Kilimo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa