Halmashauri za Mkoa wa Mbeya, GIZ na Taasisi za dini zinazoendesha Hospitali na Vituo vya Afya vilivyoingia ubia na Serikali Mkoani Mbeya wamejaza mikataba ya utoaji huduma za Afya.
Akifungua zoezi la kuandikishana mikataba,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla aliyataja madhehebu ya kidini kuwa na mchango mkubwa katika utoaji huduma kwenye Sekta za Elimu na Afya hatua aliyosema inaipunguzia kwa kiasi kikubwa mzigo Serikali.
Mhe Makalla amesema uwepo wa Hospitali,Vituo vya afya,Shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vinavyomilikiwa na Madhehebu ya kidini umeweka chachu ya utoaji huduma bora kwa wananchi.
Amesema Serikali ya mkoa itazidi kuhakikisha kunakuwepo na ushirikiano wa pamoja baina yake na Madhehebu yanayoonesha nia ya kushiriki shughuli za kijamii na iwapo tatokea kiongozi katika ngazi ya wilaya anayetaka kufifisha mahusiano hayo basi hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Amewataka pia Wenyeviti wa Halmashauri kusimamia mikataba iliyosainiwa kwa ufasaha ili kutoa wavunja moyo wadau walioamua kuingia ubia na serikali katika utoaji huduma kwa wananchi.
“Na sisi viongozi wa Serikali huko tulipo tusiwe wavivu wa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau wetu.Kama unasikia madhehebu haya ya kidini yana mgogoro wa ardhi fanya upesi kwenda kutatua maana maeneo hayao hayo wanayolumbana ndiyo watafanya uwekezaji” Mhe Makalla
Mshauri wa mpango wa PPP wa Shirika la GIZ Ndugu Erick Msoffe alisema Shirika hilo litahakikisha wadau wa Sekta ya Afya wanaohusika na mikataba iliyoingiwa baina ya pande hizo wanakutana katika kila robo ya mwais wa fedha ili kujadiliana kwa pamoja juu ya utekelezaji wa majukumu
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa