Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya halmashauri Saba za Mkoa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo hadi Mei 31, 2019 kiasi cha sh. 3, 516,444,947.00 sawa na asilimia 118.87. Mhe Chalamila ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Baraza maalumu la Kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali na kuwataka kuendelea jitihada za kukusanya ili ifikapo Juni 30, 2019 halmashauri ifikie asilimia kubwa zaidi na kuendelea kuongoza. “Hata hivyo kutokana na ukomo wa bajeti yenu, ni vema mkaandaa maelezo ya kutosha kuhusu makusanyo ya mapato ya ndani yanavyoongezeka zaidi ya mlichopanga kukusanya ili kuweka kumbukumbu zenu vizuri na kuweka uelewa wa kutosha kwa watumiaji hesabu zenu pia kumtosheleza mkaguzi anapopita kuwakagua”. RC Chalamila. Mhe Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema jukumu la ukusanyaji mapato ni la watendaji na Madiwani, hivyo hakuna budi kutumia uwezo wenu kuhakikisha kwamba mapato yanapanda na kishirikiana na wadau wengine katika kutafiti na kubuni vyanzo vipya vya mapato. Aidha, Mhe Chalamila amesema kuwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ni lazima kuendane na nidhamu ya matumizi hivyo ni jukumu la Madiwani kuhakikisha kuwa mapato yote yanakusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani na ruzuku ya Serikali yanatumika katika malengo yaliyokusudiwa. Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw Paul Ntinikaamesema kuwa anajivunia kuwa na halmashauri ambayo inashika nafasi ya kwanza kwa ukusanyaji wa mapato na kusimamia ipasavyo matumizi ya mapato hiyo na kufanya halmashauri hiyo kupata hati safi. Bw. Ntinika amesema kuwa halmashauri ya Mbeya pia imeweza kutoa zaidi ya milioni 400 za asilimia 10 kwa ajili ya kinamama, vijana na walemavu na kufanya halmashauri hiyo kutoa fedha zote za za 10% katika bajeti ya mwaka 2018/2019. Naye Mwenyekiti wa halmashauri Mhe Mwalingo Kisemba amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya watumishi wa halmashauri na Baraza la Madiwani na kuahidi kuongeza kasi hiyo ya kukusanya mapato na kubuni vyanzo vipya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa