Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amezishauri Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuanza ujenzi wa shule ya bweni kwa wanafunzi ambao hawajafanya vizuri katika mtihani wa kidato cha tatu na nne.
Mhe Chalamila amesema hayo leo tarehe 11 Februari, 2021 wakati akikagua ujenzi wa shule ya ya mchepuo wa kiingereza Kata ya Nsalaga lengo la Serikali kufanya hivyo ni kuwezesha watoto hasa wa kike waliofanya vibaya kupata fursa ya kuendelea na masomo.
"Unajua tukipata uongozi kutoka kwenye hayo majeshi sambamba na shule hiyo, pia kuwapo kwa msikiti na kanisa kwa ajili ya ibada Ijumaa na Jumapili, watoto hawatoweza kufanya vibaya ,"amesema Chalamila.
Maelezo ya mkuu wa mkoa yameungwa mkono na wakazi jijini, wakisema utawezesha watoto kufanya vizuri katika mitihani na kuepuka vishawishi ambavyo ni chanzo cha kufanya vibaya.
Mkazi wa jiji, Salina George amesema changamoto kubwa kwa watoto wa kike kufanya vibaya ni kutokana na vishawishi wanapokwenda shule na wanapotoka kwasababu ya umbali.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa