Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuandaa mpango Mkakati wa namna watakavyo lipa madeni ya watumishi hasa Idara ya Elimu na Afya ili kuweza kuondokana na madeni hayo.
Mhe Homera ameyasema hayo leo Juni 10, wilayani Kyela kwenye kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kupitia hoja za ukaguzi na kuitaka Halmashauri kuanza kulipa kidogo kidogo ili kurudisha hari ya watumishi kufanya kazi.
“ Wekeni mipango kwamba kutoka Februari 2020 hadi Machi 2021 sisi Kyela tunadaiwa bilioni 2.7, tutalipa kama ifuatavyo na itafurahi kama mtaanza kulipa watumishi wachache ili wapate nafuu na kuona matumaini” Mhe Homera
Akikamribisha Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Angelina Lutambi amewataka wakurugenzi kuhakikisha wanawalipa watumishi fedha za uhamisho mapema pale wanapowahamisha na wasiwahamishe kama hawana fedha za kuwalipa watumishi hao.
Aidha, Dkt Lutambi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanawapandisha vyeo na kuwabadilisha kada watumishi wote wenye sifa na kuhakikisha wanawaingiza kwenye Mfumo wa Kiutumishi kabla ya tarehe 12 Juni, 2021
Dkt Lutambi amesema kuwa watumishi wote waliopandishwa vyeo wanatakiwa kuingia kwenye Mfumo mapema ili kuepuka malimbikizo ya madeni na kuipa mizigo halmashauri zetu.
“Sasa wakurugenzi mhakikishe watumishi wanapandishwa vyeo kwa muda na kuingizwa kwenye mfumo hasa idara ya elimu na Afya” Dkt Lutambi
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa