Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameziagiza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya Kutelekeza Mradi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ‘Tumaini la Mama’ wenye lengo la kumkomboa Mwanamke kumpatia Huduma za Matibabu wakati wa Ujauzito.
Makalla amesema hayo wakati wa kikao cha Kazi cha kujadili Utekelezaji wa Mradi huo kwa viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Awali akizungumza wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya’ NHIF’ Bernard Konga amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu kwa mkoa wa Mbeya umeanza mwaka 2012.
Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu kwa awamu ya kwanza ulihusisha mkoa wa Tanga na kwamba katika awamu ya pili mradi huu umefika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Konga amesema kuwa sababu za mikoa hii kuwa ni ya kwanza katika mradi huu ulitokana na ongezeko la vifo vya Akina Mama na Watoto hadi kufikia 2012
Aidha wakizungumza mpango mkakati wa utekelezaji wa Mradi huo Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Kitta wamesema kuwa wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuwa umefika wakati unaostahili kutokana na changamoto zilizopo katika wilaya hizo
Aidha wakizungumza mpango mkakati wa utekelezaji wa Mradi huo Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Kitta wamesema kuwa wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuwa umefika wakati unaostahili kutokana na changamoto zilizopo katika wilaya hizo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa