Hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa mtu kutoka taasisi yoyote atakayehusika na kusababisha majanga ya moto kwenye shule za Mkoa wa Mbeya kuanzia sasa.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila leo katika shule ya Sekondari ya Panda Hill alipofanya ziara ya kukagua shule za Sekondari Wilaya ya Mbeya.
Mhe Chalamila amesema kuwa baadhi ya shule wanafunzi wanashiriki katika uchomaji wa mabweni zikiwemo shule za UWATA na Kiwanja.
" Shule ya Kiwanja wanafunzi wamechoma mabweni, nilipiga viboko na watano tuliwaweka jela, watatoka baada ya miaka minne,wakitoka nitawapeleka kambi za jeshi na magereza wafanye kazi kwa kujitolea, tukikuta mwanafunzi anachoma, atauzima kwa mikono” Mhe Chalamila.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Panda Hill Mtawa Zephania James amesema kuwa ili kujilinda na majanga ya moto shule imefuata ushauri uliotolewa na kamati ya Usalama ya Wilaya na kuanza kutumia umeme wa jua, kufunga kamera 65 kwenye maeneo ya shule na kuongeza idadi ya walinzi.
Mtawa James ameendelea kusema kuwa shule imejizatiti kuhakikisha kuwa majanga ya moto hayatokei tena na kwa sasa shule iliamua kujenga mabweni ambayo ni rafiki hata inapotokea majanga hayo wanafunzi wasiweze kuathirika.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika amesema kuwa amefurahishwa na uongozi wa shule ya Sekondari ya Panda Hill kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Usalama ya Wilaya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa