Kamati ya watu saba iliyoundwa naMkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe Albert Chalamila kuchunguza kifo cha dereva wa lori, Abrahaman Issa imebaini kuwa ugonjwa wa homa ya mapafu ndio chanzo cha kifo cha mkazi huyo wa Temeke jijini Dar es Salaam.
Mhe Chalamila ametoa taarifa ya kamati hiyo leo Jumanne Februari2, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari aliyoiunda kusaka ukweli wa kifo cha dereva huyo kilichozua utata baada ya wenzake kudai alifia kituo cha polisi huku polisi wakieleza kuwa alikufa baada ya kufikishwa hospitali na kwamba alikuwa na homa ya mapafu.
“Kamati iliyohusisha vyombo vya dola imefanya uchunguzi wa kina uliohusisha madaktari bingwa walichukua sampuli za vipimo katika kichwa na kifua ili kujiridhisha kama kunaweza kukawa na shida ambayo aidha ilitokana na kipigo au.”
“Lakini ilibainika tatizo ni homa kali ya mapafu na kabla ya kupatwa na tatizo hilo alikuwa na tatizo la pumu kwa kipindi kirefu. Unajua pumu au homa ya mapafu haistahili mtu kukaa kwenye chumba chenye baridi, licha ya afya yake kudhoofu huenda ilichangia kudhoofika zaidi na kusababisha umauti kumkuta kutokana na kukaa kituo cha polisi kwa masaa kadhaa,” amesema Chalamila.
Kuhusu sehemu aliyofariki dunia, Chalamila amesema,” kamati ilibaini afariki dunia saa 3 usiku akiwa katika gari la polisi akipelekwa kupatiwa matibabu katika kituo cha afya igawilo jijini Mbeya.”
Amesema Issa alipofikishwa katika kituo hicho daktari aliyekuwa zamu alibaini kuwa alikuwa amefariki dunia, mwili wake ulihifadhiwa.
Chalamila amesema amemuagiza kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei kugharamia shughuli zote za mazishi ya Issa.
"Nimezungumza na ndugu wa marehemu kama watakuwa tayari kuchukua mwili kwa mazishi nimetoa kibali leo na kama hawajaridhishwa na majibu ya kamati kama Serikali tutawasikiliza uamuzi wao,” amesema.
Awali mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa malori, Abubakar Msangi amesema baada ya kupatiwa ripoti hiyo ndio watatoa majibu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa