Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla amesema Mbeya umeendelea kuunga mkono jitihada hizo za Serikali kwa vitendo kwa kujenga miundombinu muhimu kwa ajili ya uwekezaji kama vile barabara, kujenga miundombinu ya umwagiliaji, umeme, kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na mengine.
Mhe. Makalla ameyasema hayo katika Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati Mkoa uliyojiwekea kama Mkoa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa wetu kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta ya umma na binafsi.
“Tunatambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kufikia uchumi wa kati. Uwekezaji huu unafanywa kwa namna mbalimbali ikiwemo ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi” Mhe Makalla
Uchumi wa Mkoa unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili, biashara, uzalishaji viwandani, utalii na ajira katika taasisi za Serikali na sekta binafsi. Hadi Kufikia mwaka 2015 kabla ya Mkoa kugawanywa na kuwa mikoa miwili ya Mbeya na Songwe, Mkoa wa Mbeya ulikuwa unachangia asilimia 7.4 kwenye Pato la Taifa ukiwa ni mkoa wa tatu baada ya Dar es Salaam na Mwanza. Hata baada ya kugawanywa, Mkoa wa Mbeya umeendelea kufanya vizuri ambapo hadi sasa Pato la Mkoa kwa mwaka 2016 lilifikia Sh. Trilioni 5.832, wastani wa Pato la mtu kwa mwaka 2016 ni Sh. 3,097,049.00 na Mkoa unachangia 5.62% ya Pato la Taifa ukiwa ukiwa ni Mkoa wa Pili baada ya Dar es Salaam.
Mhe Makalla amesema kuwa Mkoa wa Mbeya una jumla ya jumla ya viwanda 1,682, kati ya hivyo vikubwa ni 10 ambavyo ni Mbeya cement, PEPSI, Mbeya Breweries Co. Ltd, Coca cola Kwanza, Marmo E. Granito Mines (T) Ltd, Wakulima Tea Company, Katumba Tea Company, City Coffee, Tol Gases na Kapunga Rice Mills na viwanda vidogo 1,625 na viwanda vya kati ni 20.
Aidha, Mkoa umeainisha minyororo ya thamani (value chains) za kuendelezwa ambayo ni alizeti, mahindi, viazi mviringo, maparachichi, mpunga, michichikichi, kakao, kahawa na maziwa na Matokeo chanya yameanza kuonekana. Kwa mfano, tayari tumeanzisha Kongani (clusters) ya alizeti yenye viwanda 41, Kongani ya Mpunga yenye viwanda 30, Kongani ya chakula cha mifugo yenye viwanda 3 katika Wilaya ya Mbeya. Aidha, tumeanzisha Kongani ya Mpunga maeneo ya Igurusi na Ubaruku Wilayani Mbarali yenye viwanda 17 na Kongani ya alizeti Chunya yenye viwanda 19, hivyo kufanya jumla ya Kongani za 3 zenye jumla ya viwanda 107 vya kuongeza thamani ya mazao.
Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson Mkoa Mkoa una fursa za kipekee za vivutio vya utalii. Fursa za Utalii zilizopo ni pamoja kuwepo kwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa Kitulo, Hifadhi ya Mlima Asilia Rungwe, Pori la Akiba la Mpanga - Kipengere, Mapori ya Uwindaji Wilayani Chunya, Ziwa Ngosi Wilaya za Rungwe na Mbeya, Fukwe za Ziwa Nyasa na Kumbukumbu za Kihistoria. Fursa nyingine ni ujenzi wa Mahoteli, Migahawa ya kisasa na Maduka (shopping centres)
Dr. Ackson amesema kuwa Mkoa wa Mbeya uko katika eneo la kimkati kwa uwekezaji wa aina zote. Nimeeleza mafanikio yaliyopatikana kiuchumi. Maeneo ya kimkakati ya uwekezaji yameendelea kujengewa miundombinu muhimu inayochochea ukuaji wa sekta hasa kilimo ili kupata malighafi za viwanda
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda Bw Rupia amesema kuwa pamoja na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uwekezaji, bado kuna fursa kubwa ya kupanua uwekezaji katika Mkoa wetu wa Mbeya hususan katika sekta za kilimo, viwanda, utalii na madini. Malengo ya Kongamano letu la leo ni kuhamasisha, kukuza na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa, chini ya Kauli Mbiu ya “Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Mkoa Wa Mbeya”.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa