WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Suleiman Jaffo amesema ameridhishwa na jitihada za Mkoa wa Mbeya katika kupambana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa iliyosababisha baadhi ya wanafunzi waliofaulu kutochaguliwa kuanza kidato cha kwanza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa Mkoa ulikuwa ukikabiliwa na uhaba wa vyumba 33 vya madarasa kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu.
Hata hivyo,Jaffo leo amefanya ziara na kutembelea Shule ya Sekondari Ilomba iliyopo jijini Mbeya na kujionea jitihada zinazoendelea za ujenzi wa vyumba vinne vya darasa shuleni hapo ili wanafunzi 157 waliokosa nafasi waanze masomo.
Waziri huyo amesema wakati akitangaza matokeo ya ufaulu wa wanafunzi wanaopaswa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu,Mbeya ilikuwa kati ya mikoa iliyompa mashaka kutokana na kufaulisha wanafunzi wengi ikilinganishwa na vyumba vya madarasa vilivyokuwepo
Amesema kwa jitihada alizojionea na mpango mkakati aliopewa wa hadi Januari 28 wanafunzi wote wawe wameanza kidato cha kwanza mkoani hapa inadhihirisha nia ya dhati ya kuhakikisha watoto wanapata elimu.
Kwa mujibu wa,Afisa Elimu Sekondari jiji la Mbeya,Mwalimu Abu John Shule ya Sekondari ya Ilemba pekee ilipangiwa wanafunzi 400 lakini 157 kati yao hawajaanza masomo na wenzao jana kutokana na uhaba wa vyumba vinne vya madarasa shuleni hapo.
Mwalimu John amesema changamoto hiyo ndiyo iliyowalazimu wadau kuungana kwa pamoja na kuanza ujenzi wa vyumba vine vya madarasa alivyosema kuna uhakika hadi Januari 28 vitakuwa vimekamilika na kuanza kutumika.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa