Kamati ya Siasa ya Mkoa ikiongozwa na Mwenyekiti Mch. Jacob Mwakasole ameupongeza uongozi wa Mkoa pamoja na Halmashauri zake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Mchungaji Mwakasole ameyasema hayo leo kwenye majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri na kukiri kufurahishwa na ubora wa miradi waliyoikagua katika halmashauri zote saba za Mkoa wa Mbeya. “ tumefurahi kuona Viongozi na wataalamu wanatusaidia kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha kile tulichoahidi wananchi kimetekelezwa kwa asilimia kubwa na hivyo kuturahisishia majibu kwa wananchi” Mchungaji Mwakasole Mchungaji Mwakasole amesema kuwa ziara hiyo ina lengo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa na chama cha mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 kwa lengo la kujua utekelezaji wa ilani ya chama katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
“Niwapongezi kwa usimamizi mzuri wa majengo haya kwa uaminifu kwani majengo haya yanaakisi fedha zilizotolewa , watu mmefanya vitu vyenye uhakika sisi kama mkoa tumeridhika na hiki tulichokiona, umoja wenu unadhiilisha kuwa mpo vizuri, asanteni wote kwa kazi nzuri.” Mwakasole.
Naye katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya ndg. Solomoni Itunda amesema kuwa miradi hiyo itakapokamilika kipaumbele kiwe katika kuhudumia wananchi wanyonge.
“Miradi hii imejegwa kwa gharama kubwa kwa ajili ya wanyonge hivyo kama kuna mtu amekuja kutibiwa na hana fedha za matibabu atibiwe kwanza mengine baadaye na kwa upande wa wanafunzi sitegemei kuona mwalimu anamfukuza mwanafunzi kwa kosa la kutokulipa ada, mkamate mzazi wake mkubaliane ni kwa jinsi gani mtablipa hizo ada lakini si kwa kumsimamisha mwanafunzi masomo”. Itunda Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila ameishikuru kamati ya siasa kwa ushirikiano wao na kuahidi kuendelea kusimamia kwa makini zaidi miradi hiyo katika kuunga mkono juhudi za Mhe Rais John Magufuli
Katika ziara ya kamati ya CCM mkoa wa Mbeya miradi iliyotembelewa ni miradi ya Afya, Elimu, Miundombinu, Kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa