NAIBU Waziri wa Madini,Dotto Biteko ameipongeza kampuni ya Marmo Granito ya mkoani Mbeya akisema inatekeleza nia ya inayohitajika na Serikali ya awamu ya tano ya kuongeza thamani kwa madini kabla ya kuyapeleka nje ya nchi.
Biteko alimwaga sifa hizo jana alipotembelea kiwanda cha Kampuni hiyo kinachojihusisha na uongezaji samani wa mawe aina ya Mabo kwa kutengeneza samani mbalimbali na kisha kuziunza ndani na nje ya nchi.
Alisema Serikali imedhamiria kuona madini yote yanaongezewa thamani kabla ya kuuzwa nje hatua inayolenga kuleta faida zaidi kwa taifa na wawekezaji nchini.
Aliwataka wawekezaji wengine katika sekta ya madini kuiga mfano huo na kuanza kuyaongezea thamani madini yao ili waweze kunufaika nayo na pia kuipa Serikali faida tofauti na kuyauza kama malighafi.
“Kama wawekezaji wote walio na leseni za madini nchini wangefanya hivi nina imani tungepiga hatua kubwa sana.Na lazima tufanye hivi iwapo kweli tumedhamiria kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.”
“Tukibakia kusafirisha malighafi hakuna tutakachokipata zaidi ya kuwanyima watanzania wenzetu ajira na kuwapelekea wengine nchini mwao.Mwisho wa siku tutakuja kujikuta tumemakiwa na mashimo matupu na hatuna tena madini.Itakuwa ni aibu kwa kizazi cha wakati huo na watatuuliza tulifanya nini”alisema Biteko.
Naibu Waziri huyo alisema ipo haja ya kuzidi kuwapa moyo na fursa zaidi wawekezaji wanaoonesha nia ya dhati ya kutoa ajira kwa watanzania kwa manufaa ya sasa nay a baadaye kuliko wale wanaolenga kuja kuchukua rasilimani nchini na kuzipeleka kwao.
Alisema ni bora kuwa na wawekezaji wachache wenye nia inayoendana na taifa kuliko kuwakumbatia wengi wanaotaka siku moja taifa liaibike kwa kuondokewa na rasilimali zake.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa