Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava leo Jumanne tarehe 27/08/2024 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Mji wa Tukuyu unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya.
Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dtk.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza karibu huduma ya majisafi kwa wananchi hivyo miradi ya maji lazima ikamilike.
Amesema kwamba kasi ya Wizara ya Maji ni kubwa na tunashuhudia huduma ya maji inavyosogezwa kwa jamii hivyo ni uhakika kwamba mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Mji wa Tukuyu utakamilika.
" Wizara ya Maji chini wa Waziri Jumaa Aweso ina kasi kubwa ya kusogeza huduma kwa jamii nawahakikishia mradi utakamilika" amesema Ndugu Godfrey Mnzava.
Aidha, Mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Mji wa Tukuyu unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya na kutekelezwa na Mkandarasi Make Engineering and water works ltd ukihusisha kazi za kulaza bomba Kuu umbali wa km 9.5 na kulaza mabomba ya mtandao umbali wa km 20.
Pamoja na kazi hizo mradi huu unahusisha ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 1.5.
Hadi kukamilika kwa mradi huu Serikali itakua imetumia jumla ya shilingi Bilioni 4.5.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa