Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amezirejesha Kaya 309 za wananchi wa Vijiji vya Ndolela, Mapaliji na Ikawe Wilaya ya Chunya baada ya tume aliyounda kujiridhisha kwamba waliondolewa maeneo hayo kwa makosa.
Mhe Makalla ameyasema hayo leo kwenye mikutano wa hadhara Kijiji cha Shoga ambapo amesema kuwa aliunda tume baada ya kupita malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo pamoja na baraza la madiwani.
Mhe Makalla amesema kuwa tume ilibaini zoezi la kuwaondoa wananchi hao katika vijiji hivyo lilifanyika kimakosa kwa sababu wananchi walikuwa wakiishi katika eneo msitu wa Kijiji ambao walipewa kisheria kwa kupewa hati miliki za kimila zilizothibitishwa na halmashauri ya Wilaya.
Amesema kuwa zoezi hilo limeonyesha kuwa hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Serikali ya Wilaya na Kijiji kwa sababu vijiji hivyo vinatambulika kisheria na kuwa na viongozi waliochaguliwa.
Aidha, Mhe Makalla mewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuacha uvamizi katika Hifadhi, vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira na kutaka halmashauri kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya hiyo.
Akiongea katika mkutano huo Mchungaji Edson Antony amesema kuwa maaskari walicho kaya zaidi ya 300 pamoja na chakula na Mifugo yao kupelekea kupata hasara kubwa ikiwa pamoja na kuingia madeni ya ifaa vya umeme wa jua walivyokopesha
Mchungaji Antony amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuweza kuwarudisha katika maeneo yao zamani kwani sehemu walizohifadhiwa walianza kuondolewa kwa kuwa walikaa kwa muda mrefu.
Naye Bibi Justina Joseph amelalamika kuwa wakati wa zoezi yeye alikuwa na uchungu wa kujifungu hali iliyompelekea kujifungulia nje baada ya maaskari kumwondoa kwa nguvu katika nyumba yake.
Kaya 309 zilizokuwa na wananchi mmoja mmoja 1310 walitolewa katika maeneo wanayoishi kwa kudaiwa kuvamia hifdhi ya msitu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa