Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg: Abdallah Shaib Kaim amezindua Mradii Wa kisima Cha Maji Kijiji Cha Kibaoni Kata ya Iyai Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali unohudumia Wakazi Wa kaya 108 na vituo Vya Umma 14.
Katika Taarifa iliyosomwa mbele ya Kiongozi imesema Mradi huo umegharimi kiasi Cha Sh. 218'538,785.43 na kidai chanzo Cha Fedha za Mradi huu ni mapato ya Ndani ya Halmashauri ambayo imetoa Tsh: 26,324,513 na kuongezwa kiasi Cha Tsh: 192,214,272.43 Kutoka kwa Wadau mbali mbali ambao ni Water Charity kupitia mashirika ya CRS na SAWA.
Akitoa Maelezo ya Mradi mara baada ya kuukagua Abdallah Shaib ameipongeza Wizara na Mamlaka zinazohusika na Usimamizi Wa Upatikanaji Maji na ameziasa Mamlaka hizo kuendelea kuwahudimia Wananchi wote hasa katika Kutoa huduma hiyo ya Maji ambayo kimsingi ni nguzo kubwa katika Maisha ya Mwanadam
Mhandisi Maryprisca Mahundi Naibu Waziri Wa Maji amewaasa Wananchi Wa Kibaoni kutunza Vyanzo Vya Maji na ameahidi kwa niaba ya Wizara ya Maji watahakikisha wanatekeleza Adhima ya Mh: Rais ya kupeleka huduma ya Maji katika maeneo yote ya pembezoni kwa asilimia 85 pasipo kujali Umbali Wa makazi husika.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa