Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Kyela na Wadau wa Elimu kwa kuweza kuandaa Kongamano la Elimu lililofanyika kwa ajili ya kuinua ufaulu na elimu bora katika shule za Msingi na Sekondari kwa kutoa changamoto ambazo zitasaidia Serikali Wilaya ya Kyela.
Akiongea katika Kongamano hilo Mhe. Makalla amesema lengo la kongamano ni kujadili kwa uwazi changamoto za elimu Wilaya ya Kyela na namna ya kupambana nazo ili kuwe na Elimu bora kwa wanafunzi na kuwa na watu wataalamu wanaotoka katika Halmashauri hiyo.
Akielezea Changamoto zinazosababisha ushukaji wa ufaulu hasa kwa Shule za Msingi amesema kuwa kuna haja ya kuboresha upatikanaji wa Chakula shuleni. Wazazi wanatakiwa kujitoa kuhakikisha kuwa watoto hawashindi na njaa shuleni. Amesema kuwa Utafiti wa unaonyesha kuwa watoto wanaelewa masomo vizuri wakiwa wameshiba.
Aidha, Mhe. Makalla amesema kuwa upungufu hosteli za unasababisha wanafunzi kutumia muda mwingi barabarani na kuwaweka katika mazingira hatarishi wanafunzi wa kike na kusababisha. Ni jukumu la Viongozi wa Siasa na Serikali kuishawishi jamii umuhimu wa kuwa na hosteli katika shule za Mkoa wa Mbeya na kuhamasisha wananchi kuchangia kwa nguvu ujenzi wa hosteli bila kujali itikadi za kisiasa.
Akiwasilisha Taarifa ya Elimu Wilaya ya Kyela Afisa Elimu Msingi Bw. Palemone Ndarugiliye amesema kuwa kiwango cha elimu Wilayani Kyela kimekuwa kikipungua toka mwaka 2014 ambapo ufalu kwa Shule za Msingi kwa Mtihani wa Darasa la Saba.
Bw. Ndarugiliye amesema kuwa ufaulu kwa upande wa Sekondari umeporopoka kuanzia mwaka 2015 mpaka mwaka 2016 ambapo changamoto kubwa ikiwa ni upungufu wa walimu, utoro na wazazi kutokuwa tayari kuwajibika kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu.
Wakichangia hoja katika kongamano hilo wadau wa elimu Wilaya ya Kyela wameishauri Serikali ya Wilaya kuwapa motisha walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao ikiwa ni pamoja na halmashauri kutenga fedha za mapato yao ya ndani. Hii itasaidia kuleta Ushindani wa walimu na wanafunzi katika taaluma.
Pia wadau wameishauri Halmashauri kutatua changamoto zinazo wakabili walimu ikiwepo kulipa madeni yao na pia kuagawa ikama ya walimu kwa kuzingatia uhitaji wa shule husika katika halmashauri ili kupunguza upungufu wa walimu katika maeneo mengine.
Mkoa wa Mbeya umekuwa ukifanya vibaya katika matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi na Se kutoka 2014 hadi sasa na hivyo kumfanya Mkuu wa Mkoa kushauri Wilaya kuandaa makongamano kwa ajili ya kutafakari kwa uwazi na kujua changamoto za Elimu
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa