Maafisa Upelelezi wa Mikoa na Wilaya za kanda ya Nyanda za juu kusini watakiwa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa weledi katika kusimamia na kutekeleza sheria ya alama ya bidhaa yenye lengo la kuzuia na kudhibiti bidhaa bandia kwa kuimarisha uchuuzi wa bidhaa na ufanyaji biashara,ili kuboresha ushindani.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila wakati akifungua Mafunzo mahsusi kwa Maafisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mikoa na Wilaya wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini iliyo andaliwa na Tume ya Ushindani (FCC) iliyo fanyika Februari 1,2019 katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa jijini Mbeya.
Mhe Mkuu wa Mkoa alisema mafunzo hayo yataleta mabadiliko katika utendaji wa kazi wa Maafisa hao na vilevile yataleta mabadiliko Makubwa ya kiuchumi kwenye Taifa letu kwa kuwa mbinu mbali mbali zinatumika ile ziweze kumlinda Mwananchi (mlaji) dhidi ya athari na madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa bandia.
Aidha,ameishukuru na kuipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa kuandaa mafunzo hayo ya udhibiti wa bidhaa bandia nchini,ambapo yanajenga ushirikiano mzuri kwa Jesi la polisi kama wadu wa kuu katika kutekeleza sheria ya Alama za Bidhaa bandia katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika kuzuia bidhaa bandia.
“Katika nchi yetu ni lazima kuwe na bidhaa ambazo zina ubora na viwango vyake vipo sahihi na hakuna wizi wa nembo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine , na vilevile udhibiti umeimarika ili kuleta Imani kwa wawekezaji wenye nia njema wanaweza wasivutiwe kuwekeza jambo ambalo litaathiri uchumi wa Viwanda katika Taifa letu” Alisema Chalamila
Awali, Bi. Magdalena Utouh akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani katika mafunzo hayo aliomba Mtanzania mmoja mmoja na wote kwa pamoja kushirikiana katika kupambana na bidhaa bandia, kwakuwa udhibiti wa Bidhaa Bandia ni sehemu muhimu ya uimarishaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
“Uchumi jumuishi na unaotegemea viwanda hautapatikana kirahisi kama soko litakuwa limejaa bidhaa bandia.”Alisema Utouh
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa