Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri wanayoifanya, pia kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha ufaulu wa wanafunzi kuanzia darasa la saba asilimia 81.6% ya ufaulu, kidato cha nne 81% huku lengo ikiwa kufikia 90%. Kwa upande wa kidato cha pili kiwango cha ufaulu kimefikia 97%.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo kwenye kikao maalumu Cha Baraza la madiwani la halmashauri ya Kyela kujibu hoja za mkaguzi mkuu wa serikali.
Chalamila ambaye alikua mgeni rasmi.
Pia amewapongeza kwa kuendelea kupata hati zinazo ridhisha mfurulizo kutokana na madiwani kuendelea kua kitu kimoja na kudhibiti masuala ya rushwa.
Mkuu wa mkoa amewakumbusha madiwani kuendelea kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza Wigo wa mapato katika halmashauri ya Kyela, Kutumia mashine za kielectronic katika ukusanyaji wa mapato ili kuepusha ubadhilifu katika ukusanyaji wa mapato. Pia amewataka kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kulingana na makusanyo na kusisitiza kua njia mpya itakayotumika ni kila halmashauri itapata kiasi cha fedha kulingana na makusanyo yake.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kyela wakiwa kwenye kikao maalum cha kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mh. Claudia Kitta akiongea kwenye kikao hicho.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa