Mhe. Makalla ameyasema hayo wakati wa vikao na Baraza Maalum katika Halmashauri ya Mbeya na Jiji la Mbeya kwa ajili ya kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameahidi Madiwani kiwa endapo hawatasimamia utengaji wa fedha asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa Wanawake na vijana atawashtaki kwa wananchi waliowachagua
Amesema kuwa kutenga fedha hizo si jambo la hiari ni matakwa ya kisera hivyo ni muhimu madiwani wakasimamia utengaji wa fedha hizo kwa manufaa ya wananchi.
Amewataka Madiwani kusimamia halmashauri kutoa fedha kwa vikundi hadharani badala yakuzitoa kimyakimya ili kuepusha vikundi hewa vinavyoisababishia Halmashauri hasara ya kupoteza
Aidha Mhe. Makalla amewataka Madiwani kuhamasisha wananchi katika Kata zako kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mfuko huo kwa ajili ya kuwawezesha Kiuchumi.
-Amewataka pia maafisa maendeleieo ya jamii kuhakiki vikundi vitakavyopewa sambamba na elimu ya ujasiriamali na urejeshaji wa Fedha hizo
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa