Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila aimeiomba mahakama kuendelea kusimamia utolewaji wa haki kwa kutoa maamuzi yasio na mashaka na kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali katika kutasfsiri Sheria.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo hii Octoba 4, 2018 ofisini kwake alipokutana na Majaji, Mahakimu na Watendaji kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya walipofanya ziara.
Amesema kuwa mhimili kuu unapofanya hukumu inawapasa kujiridhisha na kufanya maamuzi yasikuwa na mashaka kwa kujiridhisha kiasi cha kutosha ili ile haki inayokusudiwa inapatikana na kupunguza malalamiko ya wananchi ya kutotendewa haki.
“Mhimili huu ukikengeusha haki kwa namna yoyote kwa maslahi yoyote hasara yake ni kubwa sana. Tunazungumzia watu wanaoweza kuiharibu taasisi, kama kiongozi akiwa mla rushwa wasaidizi wake wataitumia mwanya huo maana wataona hakuna mtu wa kuwakemea” Amesema Chalamila
Amefafanua kuwa masuala ya kisheria ni magumu lakini mahakama imepewa dhamana kubwa ya kuyasimamia na kuomba mahakama ijisafishe hasa kwa Watendaji wachache ambao wanaolalamikiwa kuhusu rushwa na kuuchafua mhimili huo.
Akielezea dhumuni la ziara yao Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kanda ya Mbeya Mhe. Robert Makaramba amesema kuwa kuja kufahamiana kwa kuwa Mhe Mkuu wa Mkoa ni sehemu ya uendeshaji mahakama kwa sababu ni mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Mkoa kwa kushughulikia masuala ya maadili ya mahakimu.
Jaji Makaramba amesema kuwa kuna sheria inayotuongoza ni ya mwaka 2011 inayoitwa Sheria ya Utawala wa Mahakama (Judiciary Administrative Act 2011) ambayo inaweka taratibu na wajibu wa Mkuu wa Mkoa na wajumbe wanahusika katika kamati hiyo
Aidha, Jaji Makaramba amesema kuwa kwa sasa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imeanzisha utaratibu wa kutoa Elimu kwa umma mara 3 kwa wiki ili kusaidia kupunguza malalamiko ambayo haina mipango ikiwa kuitekeleza jukumu la kusaidia nchi iendelee kuwa na amani.
Mahakama Kuu ya Kanda ya Mbeya ilianzishwa tangu mwaka 1977 chini ya Marehemu Mhe Jaji Mwakibete kwa kuungana na Mkoa wa Rukwa na baada ya Rukwa kutangazwa Mkoa ikaanzishwa mahakama yake. Kwa sasa Mahakama ya Kanda Mbeya inashughulikia na Mkoa
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa