Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla amewataka viongozi wa Halmashauri kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kuendelea kuweka vipaumbele vya ujenzi wa barabara na madaraja katika maeneo yao.
Mhe Makalla amesema Mkoa una matarajio makubwa na TARURA katika kutatua changamoto za barabara zinazozikabili Halmashauri kwa hivo madiwani na Wakurugenzi wanatakiwa kuwasaidia Wakala hao katika kutimiza wajibu wao.
Mhe Makalla amesema kuwa Serikali inatarajia kuona usimamizi mzuri wa ujenzi wa barabara na madaraja, matumizi ya mazuri ya fedha na kuona miradi inayotekelezwa inaendana na fedha inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Vijijini na Mijini.
“Ni Wakala ulioanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali sura 245 (Executive Agencies CAP 245) na kutangazwa rasmi katika Gazeti la Serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017 kwa lengo la kutekeleza majukumu ya kiutendaji zaidi kuhusu maendeleo ya barabara za Vijijini na Mijini” Mhe. Makalla.
Mhe. Makalla amesema kuwa majukumu ya kiutendaji ya TARURA ni ya ujenzi, matengenezo pamoja na menejiment ya barabara za Vijijini na Mijini majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Idara ya Miundombinu chini ya Wizara OR – TAMISEMI.
Katibu Tawala wa Mkoa Bibi Mariam Mtunguja amezitaka Halmashauri kutotumia fedha za Barabara zilizopo kwenye akaunti za Halmashauri hadi pale maelekezo maalum yatakapotelewa na Wizara husika kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa kuhamishiwa kwa wakala wa Barabara TATURA.
Bibi Mtunguja amesema kuwa Wakurugenzi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia fedha za barabara zilizobaki Halmashauri hazitumiki na kuhakikisha rasilimali zilizokuwa zimefadhiriwa na fedha za barabara zinakabidhiwa kwa Wakala wa Barabara TARURA.
Mratibu wa TARURA Mkoa Mhandisi Dustan Kishaka ameeleza kuwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini umezinduliwa rasmi tarehe 02/07/2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Mjini Dododma uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote, Wahandisi wa Mikoa, Wahandisi wa Halmashauri zote, na Wakuu wa Taasisi mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Mhandisi Kishaka amesema kuwa nia kubwa ya kuanzishwa kwa TARURA ni utoaji wa huduma endelevu ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za vijijini na mijini kwa kuzingatia misingi ya ki-biashara, ufanisi wa gharama (Cost Effectiveness), masuala mtambuka (mazingira, usalama na masuala ya kijamii) kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na ki-uchumi.
Majukumu ya TARURA yameainishwa kwenye muongozo wa utendaji kazi (Frame Work Document) wa Wakala wa Aprili 2017, aya ya 3.6, na jukumu kubwa ni Upangaji na Usimamizi wa Ujenzi, Ukarabati na Matengenezo ya mtandao wa barabara za Vijijini na Mijini pamoja na madaraja kwa kuzingatia usalama, mazingira na mambo ya kijamii kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa