MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla ameagiza wanunuzi wa Tumbaku wilayani Chunya kuacha kutumia Mfumo wa malipo kwa Dola na badala yake watumie Shilingi.
Makalla amesema kupitia mfumo wa malipo kwa Dola wapo wajanja ambao wamekuwa wakinufaika kwa kuwaibia wakulima wasio nan a uelewa wa kutosha juu ya ubadilishaji fedha kimahesabu.
Katika kikao chake na wadau wa zao la Tumbaku kilichofanyika katika kijiji cha Lupatingatinga alisema kuendelezwa kwa misamiati ya Dola kutasababisha baadhi ya wakulima kuendelea kunyonywa huku wajanja wachache wakineemeka kwa jasho la wanyonge.
“Kuna viongozi siyo waadirifu wanawapiga wananchi kupitia Dola,siyo watu wote wana elimu ya ubadilishaji fedha.Tukiendeleza Dola tutatoa mwanya kwa wapigaji,achene misamiati ya Dola wewe njoo na Shilingi kama unakwenda kuuza kwa Dola huko utajua wewe hiyo ibaki siri yako”alisisitiza
Wakati huo huo,Makalla alisema atatuma timu ya watu wake kwaajili ya kukagua matumizi ya fedha za Mfuko wa Kuendeleza Elimu wilaya ya Chunya(Chudetu) ambazo zimekuwa zikikusanywa kutoka kwa wakulima wa zao la tumbaku pekee huku wadau wengine wakiachwa.
Alisema iwapo Halmashauri inakiri fedha hizo hapo awali zilisaidia ujenzi wa shule za kata na maabara za sekondari lazima sasa itambulike zinazokusanywa kwa sasa tunapelekwa wapi wakati Serikali inatekeleza Sera ya Elimu bure.
Alisisitiza kuwa iwapo atabaini fedha zinazokusanywa zinaelekezwa kwenye matumizi mengine nje ya Sekta ya Elimu hatosita kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima walihoji iwapo Mchango wa Chudetu ni kwa nia ya kuendeleza Elimu ni kwa nini wachangie wakulima wa Tumbaku pekee huku wengine wakiachwa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa