Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango leo Agosti 1,2022 mkoani Mbeya amefungua maonesho ya sherehe za Nane nane ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya
Mhe.Dkt Mpango akiwa na Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi maonesho hayo kwa mwaka huu 2022.
Aidha Mhe.Dkt Mpango amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika viwanja vya maonesho likiwemo banda la Wizara ya Kilimo, banda la Mifugo na Uvuvi, TANAPA, NMB na banda la CRDB.
Katika hotuba yake Mhe.Dkt Mpango amepongeza maandalizi mazuri yaliyofanyika na kuwapongeza wakulima, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kwa kushiriki katika maonesho hayo.
Aidha Mhe.Makamu wa Rais amesisitiza suala la kilimo biashara na kuwahakikisha wakulima upatikanaji wa pembejeo za kilimo na mbolea, "Serikali imejipanga kuhakikisha wakulima, wafugaji wanapata pembejeo za kilimo, mbolea kwa wakati na bila usumbufu"
Makamu wa Rais ametoa rai kwa Taasisi za kifedha hapa nchini kuendeleza jitihada za kuweka masharti nafuu ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili kuongeza uwekezaji na uzalishaji katika sekta hizo na kupunguza changamoto za ajira.
Kauli mbiu ya maonesho ya Nane Nane 2022 "Ajenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa