Wakazi wa vitongoji vya Bukombe na Igumbi kijiji cha Matema Wilaya ya Kyela wameondokana na tatizo la ukosefu wa majisafi lililodumu zaidi ya miaka 10.
Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilayani Kyela, Tanu Haule amesema hali hiyo inatokana na kukamilika kwa ukarabati wa Mradi wa Maji wa Matema wilayani humo
Amesema zaidi ya sh milioni 29 zilitolewa na serikali zimetumika kukarabati wa dharura wa mfumo wa maji ulioharibika miaka ya nyuma.
Deule alibainisha hayo alipotoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alipokuwa akikagua baadhi ya vituo vya kutolea maji, kikiwemo kilichopo Soko la Samaki la Matema
Alisema ujenzi wa mradi huo ulihusisha ununuzi wa mabomba ya plastiki na viungio vya mabomba, kuchimba mitaro na kulaza mabomba urefu wa mita 900 na kutolea maji na baadaye kuunganisha majumbani.
“Fedha zilizotumika kwenye mradi huu ni serikali kupitia mpango wa ‘Lipa Kwa Matokeo’ unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza.Awali ilikadiriwa kutumika shilingi milioni 20 lakini baadaye kazi ziliongezeka na tukafikia milioni 29 mpaka kukamilisha eneo la chanzo cha maji.
“Awali wakazi wa vitongoji husika walipata wakati mgumu sana kupata maji kwa ajili ya matumizi ya majumbanina kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo kwenye mto na visima vifupi vya kuchimba. Alisema
Alisema manufaa mengine ya mradi huo ni kuboreshwa kwa usafi katika soko la samaki, Awali kulikuwa na chanagamoto kubwa hususani katika vyoo vya soko, kwani watu walilazimika kuchota maji ziwani kwa ajili ya matumizi sokoni hapo.
Meneja huyo alisema miongoni mwa changamoto zinazoukabili mradi huo ni uwepo wa njia ya watalii jirani na bomba kuu linalopitisha maji kutoka chanzo cha maji ambapo hatua hiyo inahatarisha usalama wa bomba hilo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa