Matukio ya wanafunzi kujinyonga hadi kufa yameishtua serikali ya Mkoa wa Mbeya na Kisa a ishu mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila kufika katika shule ya Sekondari ya Kutwa ya Kyela inayoongoza kwa matukio hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema mwaka huu jumla ya watu 16 wamekufa kwa matukio ya kujinyonga wakiwemo wanafunzi watano.
Akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa amesema kuwa matukio hayo yametokea katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu kwa maana ndani ya miezi tisa pekee
“ ina maana kwa tuliosoma hesabu ikifika desemba mwaka huu watu waliojinyonga watafikia 21 iwepo mambo haya yataachwa yaendelee, kwa sababu Januari hadi septemba walikuwa 16 kwa hiyo kuanzia Januari-Desemba watakuwa 20 hadi 21” Matei
Matukio ya kujinyonga yaliyoripotiwa jumla 16 ya wanafunzi yakiwa matano na wilaya ya Kyela matukio ya wanafunzi kujinyonga ni mawili.
Ambapo septemba 24 mwaka huu kitongoji cha Roma, Kata ya Mbugani Kyela Grace Majaliwa (17) mwanafunzi wa kidato cha tatu alijinyonga kwenye kenchi ya nyumbani kwao kwa sababu alifokewa na kuchapwa na baba yake mzazi kwa kujihusisha na mapenzi na kutokihusisha na madogo
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa