Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amepokea taarifa ya Kikosi Kazi kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Hifadhi ya Ruaha na Vijiji 34 vya Halmasahuri ya Wilaya ya Mbarali ikijumuisha mapendekezo ya kurejesha Mto Ruaha Mkuu kurejea katika hali yake ya asili kutiririsha maji kwa ajili ya Hifadhi ya Ruaha na Bwawa la Mtera.
Mhe. Makalla amewashukuru wananchi wa Wilaya ya Mbarali kwa kuonyesha ushirikiano kwa Kikosi kazi hicho katika kupitia upya Tangazo la Serikali Na 28 ya mwaka 2008 (GN 28) na pia kuwapongeza wajumbe wa kikosi kazi kwa kufanya kazi kubwa katika mazingira magumu kwa muda muafaka.
Mhe Makalla amekiri kupokea taarifa yenye madhumuni makubwa ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya wananchi wa Wilaya hii kutaka kujua hatima yao ya kumaliza mgogoro wa wao na hifadhi ya TANAPA.
Mhe. Makalla amewaomba wanachi kuwa watulivu na taarifa ifa hiyo itawasilishwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya(DCC), Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kuwasilishwa kwa Mhe Rais kwa ajili ya maamuzi.
Akikabidhi taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mvune amesema kazi ilikuwa kubwa na ngumu kwa sababu sehemu kubwa ilikuwa haifikiki kutokana na miundombinu ya maeneo hayo kufikika kirahisi na kusababisha baadhi ya wajumbe kutembea zaidi ya Km 10 kwa miguu kuhakikisha maeneo yote yanafikika kirahisi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa