Mkoa wa Mbeya una fursa kubwa ya kuwepo kwa malighafi za aina mbalimbali na kwa kutambua hilo Mkoa umekua ukiweka mazingira mazuri na kuzingataza fursa zake kwa wawekezaji wa ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa kwa lengo la kukuza uchumi na pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa ya Mkoa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa Mkoa umeendelea kutenga maeneo ya Viwanda kwa kila Halmashauri ambapo jumla ya hekta 2,722.55 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda.
" Mkoa una jumla ya Viwanda 2,407 kati ya hivyo vikubwa ni 63 na vidogo ni 2,34 ambapo uwepo wa Viwanda hivi Mkoa wa Mbeya umechangia ukuaji wa pato la Mkoa kutoka trilioni 2.352 kwa mwaka 2008 kufikia trillion 6.761 kwa mwaka 2015".
Mhe Makalla amesema kuwa ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda ifikapo 2025 Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri umeendelea kuwahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuanzisha Viwanda kwa kuzingatia upatikanaji wa malighafi zilizopo kwenye maeneo yao na kwa mfumo wa Kongani.
Aidha, Kuhusu Vita dhidi ya Rushwa Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa umeendelea kuimarisha mikakati kwa kushirikiana na wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambapo TAKUKURU imeendelea kutoa elimu kwa Wafanyabiashara wa mazao ya Kilimo na Usafirishaji ambapo kampeni hiyo ya Elimu ya Rushwa imewafikia wananchi wa kawaida 37,230 kwa kipindi cha Julai, 2016 hadi Februari, 2017.
Jumla ya taarifa 214 za viashiria vya Rushwa zilipokelewa ambapo 71 ziko kwenye hatua ya Uchunguzi, 143 zilifanyiwa kazi na kukamilika, taarifa 17 zilihamishiwa idara nyingine na kesi 16 zilifunguliwa Mahakamani.
Suala Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe. Makalla amesema Mkoa umeanzisha vituo mbalimbali vya kutoa Elimu kwa Vijana ili watambue madhara ya kutumia Dawa Mbalimbali zakulevya. Kwa mwaka 2016/2017 kilo 709 na gramu 475 za bangi zilikamatwa pamoja na wahalifu 423 wa bangi. Heroine yenye uzito wa gramu 326 yalikamatwa na watuhumiwa 5 walifikishwa mahakamani.
Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa umeendelea kuimarisha utoaji wa huduma za nasaha na upimaji wa hiari kwa vituo vyote Afya vya Mkoa, ambapo hadi kufikia Desemba, 2016 jumla ya watu 322,949 walipima VVU kati yao 23,908 walikutwa na maambukizi ya UKIMWI sawa na asilimia 7.4.
Mkoa umeendelea kuboresha huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) ambapo jumla ya akina mama 94,850 walipima VVU kati yao wakina mama 3,960 sawa na asilimia 4.2 walipatikana na maambukizi ya VVU na wanapata huduma kwenye vituo vya afya.
Vita dhidi ya Malaria Jamii ya Mkoa wa Mbeya imeendelea imeendelea kuelimishwa kutumia vyandarua vyenye viwatilifu vya muda mrefu ambapo jumla ya vyandarua 1,226,092 viligawiwa katika jamii na vyandarua 7,788 viligawiwa katika taasisi mbalimbali.
Aidha Mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi kuweka mazingira safi ili kupunguza Mbu wanaoambukiza Malaria. Mkoa umefanikiwa kupunguza maambukizi ya Maralia kutoka wagonjwa 157,960 kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia wagonjwa 98,835 k2wa mwak 2016.
Mwenge wa Uhuru Mkoani Mbeya utatembelea miradi ya 55 yenye thamani ya Sh. 10,823,158,922.49 ambapo kati ya miradi hiyo Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 29, kuweka Mawe ya msingi miradi 14 na kukagua miradi 12. Kati ya fedha hizo Fedha za Serikali Kuu ni Sh. 2,423,140,154.00, fedha za Halmashauri ni Sh 716,060,470.00, Nguvu ya Wanainchi ni Sh. 2,635,907,100.00, Fedha za Wahisani ni Sh. 5,040,051,198.49 na Fedha za mfuko wa Jimbo ni Sh. 8,000,000.00
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa