Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ameingia Mkataba na Wakuu wa Wilaya akiwataka kuhamasisha ujenzi wa zahanati na vutuo vya Afya na wananchi kujiunga na ya afya (CHF )
Hayo yamejiri Leo ktk kikao kazi cha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Waganga wa Wilaya na Watendaji wa Kata zote Mkoa wa Mbeya.
Mhe. Makalla amesema kuwa uboreshaji afya ya msingi ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi chama cha mapinduzi Ibara ya 49 na 50(a)i
Amesema kwamba mkataba wa uhamasishaji ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ni njia ya kuwa bana viongozi na watendaji kufuatilia utekelezaji wa Ilani kwa vitendo
-Mhe. Makalla amesema kuwa mpaka sana Mkoa wa Mbeya una Vijiji 533 na Kata 178 ni Vijiji 233 sawa na asilimia 43% ndiyo vyenye Zahanati na Vituo 25 sawa na asilimia 14% kuna vituo vya Afya
Aidha , Mhe Makalla ametangaza mashindano Vijiji na Kata vitapata MABATI ya kuezekea kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikisha Wadau na Halmashauri ktk Wilaya zote kwa Lengo kufikia mwaka 2020 zaidi ya asilimia 80% ya vijiji na kata kuwa na Zahanati na vituo vya Afya
Faida ya kuboresha afya ya msingi ni pamoja na wananchi kuwa na uhakika wa huduma ya afya, wananchi kutokutumia muda mwingi kufuata huduma ya Afya, kupunguza umbali kufuata huduma afya , huduma ya mama na mtoto Kabla na Baada ya kujifungua , kudhibiti magonjwa ya mlipuko na elimu na udhibiti ugonjwa wa ukimwi
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa