Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Amos Makalla ameongoza kikao kazi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa lengo la kuhamasisha upatikanaji wa fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa baadhi ya madarasa katika shule zilizopo Halmashauri ya Jiji Mbeya.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alieleza dhumuni la kukutana kwa umoja huo lengo likiwa uhamasishaji ili kuwesheza watoto waliokosa shule kutokana na uhaba wa madarasa wanaanza shule ifikapo januari 09 mwaka ujao.
Mh.Makalla alitoa pongezi kwa kazi nzuri iliyofanyika ya ukamilishwaji wa madawati na ukarabati wa shule ya Sekondari Iyunga alisema “Kama tuliweza kukamilisha madawati na kukarabati shule iliyoinguabasi kukamilisha madarasa haya kuminaamini ni kazi ndogo na tutaiwezatukifanya kwa ushirikiano”
Pia aliwataka waratibu wa Elimu kuhakikisha wanashirikiana na Wataalamu toka Halmashauri ya Jiji ili kuhakikisha kazi inafanyikanakumalizika kwa wakati. Aliwataka wajumbe wa Bodi za Shule,Waratibu wa Elimu kata na Kamati ya Elimu kuhakikisha wanasimamia nidhamu katika mashule ili kusaidia kizazi kijacho.
Akitoa Msisitizo wa shughuli hiyo Meya wa Halmashauri wa Jiji la Mbeya Mheshimiwa David Mwashilindi alizungumza kwa niaba ya madiwani nakusema atahakikishawa nakuwa mabaloz iwazuri kwa wananchi ili kuwezesha upatikanaji wa fedha ili kuharakisha zoezi hilo nakuwezesha wanafunzi kuingia mashuleni kwa wakati.
Nae Mkurugenzi wa Jiji NduguZ.Nachoa alisema Halmashauri ya Jiji imepang kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila kata zilizo na upungufu wa madarasa ili kuwezesha zoezi hilo kuanza mara moja.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya,Madiwani, Mkurugenzi wa Jiji ,Katibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Shule za Sekondari,Wakuu wa bodi za Shule,Waratibu wa Elimu Kata pamoja na Watendaji wa Mitaa kilichofanyika tarehe 6 Disemba 2016 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji.
Halmashauri ya Jiji inajumla ya shule za sekondari 54 zikiwepo 31 za serikali na 23 za binafsi. Kwa mwaka 2016 jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi ni 9,450 waliofaulu ni 6,613 kati ya hao waliochaguliwa kujiunga na shule za bweni ni 16, waliochaguliwa kujiunga na shule za kutwa ni 6,245 waliobaki kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa ni 352.
Kati ya hawa ambao hawakupata nafasi kutokana na uhaba wa madarasa ni kutoka shule za sekondari 8 ambazo ni Sekondari ya Sinde, Sekondari ya Ihanga ,Sekondari ya Iyela, Serikali ya Mwakibete, Sekondari ya Mponja, Sekondari ya Uyole, Sekondari ya Itezi na Sekondari ya Lyoto. Mahitaji ya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza 2017 ni madarasa 166.Aidha madarasa yaliyopo ni 156 na kuwa na upungufu wa madarasa 10.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa