KMkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa Uchumi wa Mkoa umeendelea kuimarika ambapo ambapo hadi sasa Pato la Mkoa kwa mwaka 2016 lilifikia Sh. Trilioni 5.832
Akiongea katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Mhe Makalla amesema wastani wa Pato la mtu kwa mwaka 2016 ni Sh. 3,097,049.00 ambapo Mkoa unachangia 5.62% ya Pato la Taifa ukiwa ni Mkoa wa Pili baada ya Dar es Salaam.
Mhe Makalla amesema kuwa Mkoa unatekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo inalenga kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ambao kwa sehemu kubwa utakuwa ni uchumi wa viwanda.
“ Mipango ya Serikali ya kufikia lengo hilo ni pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21 ambao Serikali ya Awamu ya Tano imeamua uwe na dhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu (Nurturing Industrialisation for Economic Transformation and Human Development).” Mhe Makalla
Naye Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uwezeshaji Bw. Enock Nyasebwa amesema kuwa Serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004. Madhumuni ya Sera ni kuwashirikisha kikamilifu wananchi katika shughuli za uchumi. Sera ya Uwezeshaji inajumuisha wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi na wafanyabiashara katika sekta mbalimbali na makundi mengine.
Bw. Nyasebwa amesema hadi sasa Mkoa umeanzisha madawati ya Uwezeshaji Wananchi katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri yanayoratibu shughulizi za kuwawezesha wananchi kuhusu mitaji, stadi za biashara, masoko, miundombinu ya kiuchumi, ushirika na ardhi. Aidha, Madawati ya Uwezeshaji Wanawake kiuchumi yameanzishwa katika Halmashauri za Kyela, Rugwe, Mbeya Jiji, Mbeya na Chunya
“Mkoa unaendelea kuyatumia madawati haya kuwafikia wananchi taarifa muhimu kuhusu biashara na uwekezaji hususani ushiriki katika uanzishaji Viwanda Vidogo ili kufikia Uchumi wa kati kwa kauli Mbiu ya Mkoa wetu, Viwanda vyetu, Wilaya Yetu Viwanda Vyetu, Kata yetu viwanda vyetu, kijiji/mtaa wetu viwanda vyetu, kaya yetu viwanda vyetu.” Bw. Nyasebwa
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa