Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewapongeza wadau wa Elimu waliojitokeza katika Kongamano la Elimu Mkoa lililofanyika kwa ajili ya kuinua ufaulu na elimu bora katika shule za Msingi na Sekondari kwa kutoa changamoto ambazo zitasaidia Serikali.
Akiongea katika Kongamano hilo Mhe. Makalla amesema lengo la kongamano ni kujadili kwa uwazi changamoto za elimu Mkoa wa Mbeya na namna ya kupambana nazo ili kuwe na Elimu bora kwa wanafunzi na kuwa na watu wataalamu wanaotoka katika Mkoa wa Mbeya.
Akielezea Changamoto zinazosababisha ushukaji wa ufaulu hasa kwa Shule za Msingi amesema kuwa kuna haja ya kuboresha upatikanaji wa Chakula shuleni. Wazazi wanatakiwa kujitoa kuhakikisha kuwa watoto hawashindi na njaa shuleni. Amesema kuwa Utafiti wa unaonyesha kuwa watoto wanaelewa masomo vizuri wakiwa wameshiba.
Aidha, Mhe. Makalla amesema kuwa upungufu hosteli za unasababisha wanafunzi kutumia muda mwingi barabarani na kuwaweka katika mazingira hatarishi wanafunzi wa kike na kusababisha. Ni jukumu la Viongozi wa Siasa na Serikali kuishawishi jamii umuhimu wa kuwa na hosteli katika shule za Mkoa wa Mbeya na kuhamasisha wananchi kuchangia kwa nguvu ujenzi wa hosteli bila kujali itikadi za kisiasa.
Wakichangia hoja katika kongamano hilo wadau wa elimu Mkoani Mbeya wameishauri Serikali ya Mkoa kuwapa motisha walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao ikiwa ni pamoja na halmashauri kutenga fedha za mapato yao ya ndani. Hii itasaidia kuleta Ushindani wa walimu na wanafunzi katika taaluma.
Walimu wana changamoto zao zisipotafutiwa ufumbuzi zitarudisha nyuma elimu. Hakuna uhusiano mzuri kati ya Viongozi wa Elimu na walimu na kuwalipa madeni walimu yanaohusiana na halmashauri ambayo yapo ndani ya uwezo wao.
Naye Kaimu Meya wa Halmashauri ya Jiji Mhe. Lucas Mwampiki amesema kuwa kuna mahusiano duni kati ya walimu na jamii. Wazazi hawapo tayari kufika shuleni kupata taarifa za maendeleo ya watoto wao shuleni ambapo unawakatisha tamaa walimu,
Mhe. Mwampiki amesema kuwa wazazi wanatakiwa kukaa pamoja na watoto wao kujua matatizo yao ambayo watoto hawawezi kuwaambia watu wengine wa kuwasaidia. Ukatili wa wazazi unasababisha kupunguza uelewa wa wanafunzi darasani.
Naye Mdau wa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Ipini wa Ipini ameshauri Serikali ya Mkoa kuandaa Mfuko wa Elimu na kuweka utaratibu mzuri wa utumiaji wa fedha hizo. Wananchi wanatakiwa kuhamasishwa kuchangia masuala ya elimu kama wanavyochangia shughuli nyingine za kijamii.
Mkoa wa Mbeya umekuwa ukifanya vibaya katika matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi kutoka 2014 hadi sasa na hivyo kumfanya Mkuu wa Mkoa kuandaa kongamano hili kwa ajili ya kutafakari kwa uwazi na kujua changamoto za Elimu
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa