Mashindano ya Mbeya Super Cup yaliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera tarehe 19/08/2021 hatimaye yamefika tamati tarehe 25/8/2021. Mashindano hayo yameweza kuhusisha timu kutoka halmashauri zote za Mbeya ambazo ni Halmashauri ya Rungwe, Halmashauri ya Kyela, Halmashauri ya Chunya, Halmashauri ya Busokelo, Halmashauri ya Mbarali na Halmashauri ya jiji la Mbeya. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kutafuta vipaji kwa Mkoa wa Mbeya ili kuweza kuzipa usajili timu za ligi kuu na daraja la kwanza zikiwepo Prison fc, Mbeya city fc, Mbeya kwanza na nyinginezo na kuunda timu ya mkoa kutokana na mashindano hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Juma Zuberi Homera amemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia suluhu Hassan kwa kuweza kuendeleza michezo nchini ili kuweza kukuza vipaji kwa vijana, na pia amemshukuru Mbunge wa jiji la mbeya Dr Tulia Aksoni na wabunge wengine kwa kutoa jezi kwa timu ambazo zinatoka katika majimbo yao na viongozi wa wilaya zote za Mbeya na Mstahiki Meya mheshimiwa Dormohamed Issa Harmat na Mkurugenzi wa jiji l Mbeya kwa kushiriki na kukubali mashindano hayo yafanyike katika jiji la Mbeya.
Mheshimiwa Juma Zuberi Homera ametoa hamasa kwa vijana mbalimbali kuwa mashindano haya ni endelevu kwa kila mwaka kwa lengo la kuwapa fulsa vijana kuonesha vipaji vyao katika ligi kuu au madaraja ya chini maana inawapa vijana hali ya kupambana ili kufikia malengo, amesema hayo baada ya kuwakabidhi kombe washindi wa mashindano hayo timu ya uyole Worriors baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Kyela Combine kwa goli moja kwa sifuri.
Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Anjelina hakusita kuishukuru kamati ya mashindano ya Mbeya Super Cup ambayo yalisimamiwa na Mkurugenzi wa jiji la Mbeya mheshimiwa Amede Ng’wanidako pamoja na Meya wa jiji la Mbeya mheshimiwa Dormohamed Issa Rahmat ambao wameweza kuiongoza kamati nzima ya mashindano na kuweza kufikia tamati tarehe 25/8/2021 na pia Mheshimiwa Bi. Anjelina amewashukuru wadhamini wote kwa kudhamini mashindano haya na kuwashukuru wanahabari wote ambao waliweza kushiriki katika kutangaza na kusambaza taarifa za mashindano hayo ambayo bila wao wasingepata pongezi kwa Halmashauri nyingine
Mashindano hayo yaliweza kutamatika hapo tarehe 25/08/2021 kwa kuweza kuhusisha timu nane za kutoka Halmashauri zote za Mbeya na kupata mshindi kutoka Halmashauli ya mbeya jiji la Mbeya kwa timu ya Uyole Worriors na kufanikiwa kuchukua kombe lenye thamani ya 500,000/= na fedha tasilimu 5,000,000/= na mshindi wa pili Kyela combine wamepata fedha taslimu 3,000,000/= na mshindi wa tatu Mbeya Dc wamepata fedha taslmu 2,000,000/=
Mashindano hayo yameweza kuibua vipaji vya wachezaji thelathini na sita na pia Mkuu wa Mkoa amesema watakaa kambini na kufanya mchujo tena na kutafuta wachezaji ishirini na tano kwa lengo la kupata timu iliyokamilika kama timu ya mkoa. Mashindano hayo yatafanyika kila mwaka na kwa mwaka utaofuata kila wilaya itafanya mashindao ya wilaya kujumuisha Kata zao na kutoa timu ambazo zitajumuika katika mashindano ya Halmashauri zote na kutoa timu ya Mkoa wa Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa