Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imesema kuwa itafanya ufuatiliaji wa matunzo ya miche 100 iliyopandwa katika Shule ya Msingi Magufuli Mchepuo wa Kiingereza.
Kamishna Msaidizi wa uhifadhi Kanda ,Cosmas Ndakidemi amesema leo Desemba, 9 katika maadhimisho ya siku ya uhuru na kwamba jumla ya miche 1,000 imepandwa katika wilaya za Mkoa wa Mbeya.
Ndakidemi amesema kuwa kwa leo wamepanda miti 100 katika shule ya Msingi Magufuli ikiwa ni uzinduzi wa ugawaji wa miche bure kwa wananchi lengo ni kuhakikisha mazingira ya Jiji la Mbeya na makazi ya wananchi yanatunzwa na kuwa kijani.
"Miche hii tumetoa bure na tunakaribisha mashirika taasisi kujitokeza kuchukua na kupanda lengo ni kuweka mazingira ya Jiji la Mbeya katika hali ya kijani na hadhi ya Green city kama miaka ya nyuma na kuhamasisha jamii kuitunza "amesema.
Aidha amesema kuwa pia TFS watafanya ufuatiliaji wa hali ya ukuaji wa miche kila wakati ili kuboresha mvuto wa mazingira katika shule hiyo.
Akizunguzma mara baada ya kupanda miche ya miti 100 katika Shule hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amewaagiza walimu wa shule hiyo kila mmoja kupanda miche ya matunda na kubandika kibao chenye utambulisho wa jina la
"Nimetoa agizo hilo kwa makusudi nahitahi mnapozungumzia afya bora na ulaji wa matunda uende kwa vitendo watoto wanapokuwa shule muda wa mapumziko Wale matunda kwa wingi ikiwa ni pamoja na mbogamboga "amesema.
Aidha kwa upande mwingine ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kutenga maeneo ya kilimo cha mbogamboga na matunda kwa kutambua kuwa afya ya binadamu inalinda na ulaji wa mboga na matunda .
Pia ametumia fursa hiyo kuonya wazee wanaiongiza migogoro ya ardhi wakati serikali inawekeza miradi ya Maendeleo hususan ujenzi wa shule za kisasa michepuo ya kiingereza.
"Kuna wazee hapa mjini wanaishi kwa utapeli na kupora maeneo ya wazi sasa nitanyooka na nyinyi kikubwa tumieni busara kwani maendeleo tunayoleta ni kwa ajili ya watoto wenu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa