Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu ameupongeza Mkoa wa Mbeya kwa kuweka mikakati iliyosaidia kupunguza tatizo la Ugonjwa wa Kipindupindu hasa Wilaya ya Kyela.
Waziri Mwalimu ametoa kauli hiyo Leo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa Mbeya Mh Albert Chalamila kabla ya kuanza ziara yake ya siku moja jijini Mbeya , amesema Mkoa wa Mbeya umepiga hatua kubwa katika kupambana na ugonjwa huo .
“Muda mrefu sasa sijasikia uwepo wa ugonjwa huu hasa katika Wilaya ya Kyela ambako ndio kemekuwa na tatizo la muda mrefu kweli mnastahiri pongezi katika hili.”Amesema Waziri Mwalimu.
Aidha ameutaka Mkoa Mbeya kuweka mikakati ya pamoja itakayo saidia kudhibiti ugonjwa wa ebora endapo kutakuwepo na dalili zake hasa kutoa elimu kwa wananchi maeneo ya mipakani.
“Mh Mkuu wa Mkoa anzeni sasa kuweka mikakati ya pamoja kudhibiti hali hii endapo itatokea,niwaambieni ukweli ugonjwa huu ni hatari sana endapo utaibuka mtaacha kila kitu na kuanza kushughulika na ugonjwa huu.”Amesema Ummy Mwalimu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert amemuakikishia Waziri Mwalimu kuwa Mkoa wa Mbeya uko salama nakwamba wamejipanga katika kudhibiti hali yotote ya hatari hasa katika kupambana na ugonjwa huo .
Amesema jitihada ambazo wanaendelea nazo kwa sasa ni kutoa elimu kwa wananchi kwa maeneo muhimu hasa Mipakani pamoja na Uwanja wa Ndege Songwe.
Mwisho .
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa