NAIBU Waziri wa Madini,Dotto Biteko amewataka wakazi wa vijiji vilivyopo jirani na mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira wilayani hapa kuwa watulivu na kuwahakikishia kuwa mgodi huo utafufuliwa na watapata ajira kama zamani.
Mhe.Biteko alisema hayo katika nyakati tofauti alipokuwa wilayani Kyela na Ileje baada ya kutembelea mradi huo na kujionea uwekezaji uliofanyika wakati mgodi huo ulipokuwa ukifanya kazi.
Miongoni mwa maeneo ambayo naibu waziri huyo alilazimika kuzungumzia mikakati ya Serikali ni pamoja na alipokutana na wakazi wa vijiji jirani walioomba kujua hatima ya mgodi huo sambamba na maslahi ya waliokuwa wafanyakazi wakati ulipokuwa ukifanya kazi aliokutana nao wakati akitoka mgodini hapo.
Wananchi hao waliokusanyika getini waliomba Serikali kuufufua mgodi huo wakisema kutofanya kazi kwa mgodi huo kumewasababishia kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambapo baadhi yao wamelazimika kujiingiza katika ujangili wa uchomaji mkaa hatua inayohatarisha misitu ya asili.
Hata hivyo naibu Waziri alisema nia ya Serikali ni kufufua mradi huo hivyo wakazi wa maeneo ya jirani hawana budi kuwa watulivu wakati jitihada mbalimbali zikifanyika.
Aidha Biteko aliagiza uongozi wa mgodi uliopo hivi sasa kutoaa kipaumbele kwa wakazi wa maeneo ya jirani kwa kuwapa ajira za muda zikiwemo za kufanya usafi ndani ya mgodi huo pale Serikali inapotoa fedha ili wazidi kushiriki katika kulinda mali za umma zilizopo kwenye eneo hilo wakati jitihada za kufufua mgodi zikiendelea kufanyika.
“Tunapenda mtambue kuwa huu ni moja kati ya migodi mikubwa ambayo Serikali kamwe jhaiwezi kuiacha ikafa.Kuweni na subra kama ambavyo mmekuwa watulivu kwa muda mrefu.Tuna wahakikishia hakuna aliye na haki taachwa asilipwe hapa.Na tunawahakikishi mgodi huu lazima ufufuliwe.Tungekuwa hatuna nia ya kuufufua tusingekuwa na sababu ya kuharibu mafuta ya Serikali kuja huku”
“Lakini pia nimeagiza uongozi,Serikali inaleta fedha hapa kwaajili ya shughuli ndogondogo wakati tukiendelea kufanya jitihada za kufufua mgodi.Hizi kazi wawape ninyi miliopo jirani ili walau kasungura haka kadogo na ninyi mkafaidi wakati tunaendelea na mambo mengine.Sasa sasa hata hiki kidogo tunacholeta nacho msipate,itakuwa si haki na Serikali yetu haitaki hivyo.”alisisitiza Biteko.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kyela, Mhe Claudia Kita na mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude walisema wakazi wa wilaya hizo mbili wana uchu wa kuona mgodi huo unafufuliwa na kuanza kufanya kazi ili waweze kunufaika nao kama ilivyokuwa awali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Mhe Dk Hunter Mwakifuna alisema kufufuliwa kwa mgodi huo kutapunguza changamoto ya uhaba wa ajira uliopo katika wilaya hizo mbili na kuwa Serikali nayo itanufaika kwa kiasi kikubwa hasa kutokana na uwepo wa Meli kubwa mpya katika ziwa Nyasa zitakazotumika kusafirisha makaa yam awe kwende nchi jira
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa