Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Beno Malisa ameomba madhehebu mbalimbali ya dini yaliyopo Mikoa ya nyanda za juu kusini kuwasisitiza waumini wao kufanya ibada ya kusamehe hasa kwa waliopo kwenye ndoa ili kuzinusuru ndoa nyingi kuvunjika.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Kongamano la Kanda la Kukithiri kuvunjika kwa ndoa katika Jamii lililondaliwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) nakufayika katika Ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya Kongamano lililokusanya wadau mbalimbali ikiwemo dawati la jinsia, jeshi la Polisi na Kadhi wa Mikoa ya Nynda za Juuu Kusini.
Aidha Mh. Malisa amesema kuwa ndoa nyingi za vijana wa sasa huwa hazidumu kwa kukosa mafundisho ya mara kwa mara yatakayowafanya kuwa na uvumilivu na kusamehe.
kwa upnade Mwingine Malisa amewahakikishia waandaaaji wa Kongamano hilo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Viongozi wa dini na kuendelea kuliombea Taifa na Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa