Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Homera amemwagiza Afisa Elimu Mkoa kumchukulia hatua za kinidham Mwalimu wa shule ya Sekondari Loleza; Sabina Haule kwa kosa la kuwalaza Darasani Wanafunzi wa kidato cha sita kwa kile anachodai ni watukutu.
RC Homera amesema Mwl. Haule alifunga bweni la Wanafunzi hao na kisha akawaamuru kulala darasani. "Wewe uliamua kufunga Bweni makusudi na kisha ukaondoka na ufunguo pasipo kujali hali ya kiafya ya watoto hawa na ukizingatia Mbeya kuna baridi kali, ukawalaza Darsani ila wewe ukaenda kulala zako nyumbani", alisema Mh. Homera.
Aidha RC Homera amewapongeza Walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini licha ya kazi hiyo ni vyema wakawajali na kuwapenda wanafunzi wao. Kwa Upande wake Mkuu wa Shule ya Loleza amesema taarifa aliipata na tayari alikuwa ameshaanza utekelezaji wa namna ya kulitatua jambo hilo.
Mwalimu Sabina Haule alipoulizwa kuhusu Madai hayo ya kuwalaza wanafunzi Darasani amekana Madai hayo. "Hapana Mkuu mimi sikuwambia walale Darasani niliwambia wakalale kwenye Mabweni mengine", alisema Mwl. Sabina. "Mkuu Wale wanafunzi ni watukutu sana mara nyingi wanajifichaga uvunguni na wana vurugu saana lakini Naomba Unisamehe kama hilo ni kosa" aliongeza kusema Mwl. Sabina
Wanafunzi waliolazwa Darasani ni wa kidato cha sita mchepuo wa HGL. Ikumbukwe kuwa, Shule ya sekondari Loleza ni moja kati ya shule za Wasichana zinazopatikana jijini Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa