Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewaasa watafiti, watoa huduma na wananchi kutumia kituo Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Mbeya kutatua matatizo ya afya yanayowakabili wananchi katika Nyanda za Juu Kusini.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo 19 Novemba 2020, kwenye maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo nchi Tanzania na kuwataka watoa huduma kutumia matokeo ya tafiti katika kufanya maamuzi na kuandaa mipango ya Huduma za Afya za Wilaya na Mikoa.
Amesema kuwa huu ni mfano tosha wa maboresho makubwa yanayofanywa na kituo cha Mbeya kwa kufanya kazi kubwa ya kuimarisha matokeo ya utafiti ambayo ndiyo yanatusaidia kupata tiba, dawa na chanjo bora.
“NIMR imefanikiwa kufanya tafiti muhimu sana zilizochangia kuboresha au kutoa taarifa zilizopelekea kuboresha huduma za kudhibiti UKIMWI na magonjwa nyemelezi , magonjwa ya kitropiki yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Malaria, Kifua Kikuu, Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto na Saratani ya shingo ya kizazi na magonjwa yasiyoambukizwa katika maeneo ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi” Mhe. Chalamila
Aidha, Chalamila amemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuri kwa kuendelea kuboresha na kuweka mkazo katika sekta ya afya kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika kituo chetu hiki cha Mbwya
“Nimepata muda wa kutembelea moja ya maabara ya kituo hiki na kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Tanzania pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo. Maabara hii ina vifaa vya kisasa kabisa na ithibati (accreditation) ya kimataifa ambapo ziko maabara mbili tu Afrika nyingine ikiwa Uganda zenye Ithibati ya namna hii” Chalamila
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR ambaye pia ni Mkurugenzi Mratibu wa Taarifa na Mawasiliano ya Kitafiti NIMR, Dkt Ndekya Oriyo taasisi ilizaliwa baada Serikali kuona uhitaji wa kuwa na chombo cha kisayansi kwa ajili ya utafiti na kwa sasa taasisi ina vituo vikubwa saba na vituo vidogo saba.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Osmunda Mwanyika ameipongeza NIMR kwa jitihada zao toka mwaka 1980 mpaka sasa za kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya halmashauri hadi mkoa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa