Kipunji (rungweceubus kipunji) ni jamii mpya ya nyani waliogunduliwa mnamo mwaka 2003, ni aina ya tumbili wanaopatikana na kuishi katika misitu ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Wanasayansi waliwaita jamii hii mpya Rungweceubus kutokana kwamba wanapatikana katika mlima Rungwe na maeneo mengine yanayoizunguka milima hiyo tu.
Kipunji ambaye aligunduliwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya mazingira na viumbe hai(WCS) mwaka 2003 katika msitu mlima Rungwe ambao uko juu km 2,981 kutoka usawa wa bahari ni moja kati ya hifadhi za asili ambayo rasilimali pekee ya Taifa inayohitaji kutunzwa mazingira yake.
Nyani Kipunji kuwa ni mnyama mwenye aibu ambaye kumuona kwake kunahitaji tahadhari na inawezekana kwa siku mbili au tatu asionekane ingawa kuna wakati hutembea kwa makundi.
Kipunji anakula vyakula vya aina tofauti vikiwepo majani machanga na yaliyokomaa, maua, Matunda mabichi na yaliyoina na mazao ya shambani kama Mahindi, Viazi nk.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa