Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewapongeza Wananchi, Wadau wa Elimu, na Walimu Mkoani Mbeya kwa kuwezesha matokeo mazuri ya Mitihani ya Kitaifa ya Kidato cha Nne na Darasa la Saba na Mitihani ya kujipima ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne.
Ameyasema hayo katika Kikao cha Elimu ya Mkoa kilichoandaliwa kwa ajili ya kupongeza Wadau wa Elimu kwa kuwezesha Mkoa kupanda kutoka nafasi ya 13 hadi ya 6 kwa mtihani wa Kidato cha Nne na nafasi ya 22 mpaka 17 kwa matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2017.
Amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya kwa kuonyesha ushirikiano Mkubwa wa kutatua changamoto za Elimu Mkoa wa Mbeya hasa katika masuala ya ujenzi wa madarasa, kuweka mahusianao mazuri na walimu na kusimamia wanafunzi kwenda shule na kupunguza Idadi ya utoro mashuleni.
Mhe Makalla amesema kuwa matokeo hayo yamekuja baada ya kuandaa Kikao cha Wadau mwaka jana kuangalia jinsi ya kubadilishana mawazo na uzoefu pia kuangalia changamoto zinazoikuta sekta ya Elimu Mkoa wa Mbeya.
“Tulikubaliana suala la elimu lipewe kipaumbele kuanzia ngazi za Kijiji hadi ya Wilaya kwa kuweka iwe ajenda muhimu katika vikao mbalimbali vya maendeleo na pia kujenga mahusiano mazuri kati ya wazazi, wananafunzi na Walimu” Amesema
Mhe. Makalla amesema kuwa hataharakisha kuwavua madaraka waratibu wa Elimu au Walimu wa kuu kwa kupata matokeo mabaya kwa sababu changamoto nyingi ndani ya sekta ya Elimu zinahusisha hasa wananchi na Serikali na kusema madaraka yatavuliwa kwa Walimu na Waratibu pale tu watakaposhindwa kutimiza majukumu yao.
Dr. Tulia AcksonNaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemshukuru Mkoa kwa kazi nzuri inayofanyika hapa Mkoani hasa kwa kutambua juhudi za wananchi, Walimu na Wadau wa Elimu katika kuwezesha mkoa kupata matokeo mazuri katika mitihani ya Kitaifa.
Dk Ackson amesema kuwa kama mdau wa Elimu atahakikisha anashrikiana na Mkoa kuendelea kutambua juhudi za wananchi, Wadau wa Elimu na Walimu na kwa kuanza Tulia Trust imewapa zawadi ya fedha taslimu Wanafunzi waliongoza kufaulu Kimkoa na Shule zilizoongoza Kimkoa
Naye Bw. Ndele Mwaselela Mdau wa Elimu amemshukuru Mkoa kwa kutambua michango wanayoitoa katika ujenzi wa madarasa na utoaji wa Vifaa vya Elimu kwa shule za Mkoani Mbeya na kuahdid kuendelea kushirikiana na wananchi kuwezesha Mkoa kupata matokeo mazuri zaidi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa