Mkuu wa Mkoa Amos Makalla Mbeya ameliagiza Jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa mabasi yanayofanya safari za mikoani na wilayani pamoja na kupima kiwango cha ulevi ,kukagua leseni halali za udereva ili kuthibiti matukio ya ajali za barabarani.
Makalla, alisema jana alipokuwa akifungua mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na kwamba kama
Serikali imeshtushwa na ajali mbaya iliyotokea katika Kata ya Mwansekwa jijini hapa na kusababisha vifo vya watu nane papo hapo.
"Kwa kweli ni jambo la kusikitisha wiki moja kuna matukio matatu ya ajali za barabarani sasa ufike wakati jeshi la polisi kuonyesha makucha kwa kuwachukulia hatua madereva wazembe kwani ajali zote zinatokana na uzembe na ulevi wa madereva wawapo safarini"alisema.
Aidha aliwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kutotoa ajira kwa watu wasiokuwa na sifa kwa maslahi mapana ya taifa na kunusuru ajali na vifo visivyo vya lazima.
"Changamoto kuna baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri wamekuwa wakitoa ajira kwa watu wasiokuwa na sifa kwa kutanguliza maslahi sasa katika hilo kama serikali tunaliwekea mkakati wa kukabiliana nalo ili kuwa na madereva walio na sifa "alisema.
Makalla, pia ameonya madereva kutokiuka sheria za usalama barabarani na badala yake watumie busara ya kutambua kuwa wamekuwa wakisafirisha roho za watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO) Leopord Fungu alisema wameanza kufanya ukaguzi na zoezi bado linaendelea katika vituo vyote vya mabasi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa